De Aller-Bedste Bøger - over 12 mio. danske og engelske bøger
Levering: 1 - 2 hverdage

Bøger af Enock Maregesi

Filter
Filter
Sorter efterSorter Populære
  • af Enock Maregesi
    373,95 kr.

    Hii ni riwaya ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya inayozu-ngumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kud-hibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC); na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko.Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighai ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifia ya Magharibi - na duniani kwa jumla.Ukisoma kitabu hiki utajiuliza, "mwandishi huyu aliwezaje kusuka riwaya inayoufanya moyo kukuenda mbio, hata kukulazimu wakati mwingine kukiweka kitabu kando ili urudishe pumzi! Ukishakianza tu, hutakiacha kabla ya kujua mwisho wa vita hi kali ya kimataifa. Na kivutio kikubwa ni kuwa kiongozi wa vita hiyo kwa upande wa Umoja wa Mataifa ni Murphy Ambilikile, Mtanzania - Willy Gamba wa Karne ya 21.Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa wasomaji wa riwaya za kiswahili.Enock Maregesi ni gwiji wa vandishi wa riwaya za kijasusi na Kolonia Santita, imeweka kiwango kipya cha juu kitakachowaumiza vichwa waandishi wengine katika kutaka kukifkia.

  • af Enock Maregesi
    298,95 kr.

  • - Laana YA Panthera Tigrisi
    af Enock Maregesi
    538,95 kr.

  • - Laana YA Panthera Tigrisi
    af Enock Maregesi
    323,95 kr.

    'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya ¿ na kung¿oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi ¿ na duniani kwa jumla.Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; nikuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda ¿ na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili ¿ na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.